Posts

MATOKEO YA FATIMA

(a)   Bikira Maria   alitokea Fatima   kwa mara ya kwanza 13/5/1917   na aliendelea kutokea mara sita mfululizo hadi 13/10/1917 alipotokea kwa mara ya mwisho. TOKEO LA I – Mei 13 1917 Ujumbe- ·         Kujitoa kwa ajili ya Mungu ·         Kupokea mateso kwa ajili ya malipizi ya dhambi nyingi za kumkosea Mungu na utukufu wake. ·         Kuomba kwa ajili ya wongofu wa wakosefu Ref. Book – “ FATIMA; A MESSAGE MORE URGENT THAN EVER” pg. 31-36 TOKEO   LA   II – Juni 13 1917 Ujumbe- ·         “Yesu anataka kuanzisha ibada kwa Moyo wangu safi, ninaahidi ya kwamba watu watakaoifuata wataongoka. Roho zile zitampendeza Mungu sana kama maua ninayopeleka kwa kiti chake cha enzi Msikate tamaa sitawaacha ninyi. Moyo wangu safi utakuwa tegemeo lenu   katika maisha yenu ya mbele na njia itakayowaongoza n...

ROZARI TAKATIFU

                                                          Historia Rozari ni taji la Mawaridi.Ni neno la kilatini lenye maana ya Bustani ya maua ya waridi. Rozari inahusishwa na Zaburi 150 ambazo Wayahudi walizitumia kama sala hekaluni. Karne ya 12 walizuka wazushi wapinga dini, walioitwa Waalbigensia. Hawa walienea Kusini ya Ufaransa na Kaskazini ya Italia. Baba Mtakatifu wa wakati huo alimteua Padre Dominiki awahubirie.   Aliwahubiria kwa maarifa yake yote lakini walizidi kushupaa na kumdhihaki. Mt.Dominiki alipoona kuwa uzito mkubwa wa dhambi walizotenda watu unazorotesha kuwageuza Waalbigensia, alikwenda msitu wa Toulouse na kusali mfululizo kwa siku tatu usiku na mchana.   Akiwa msituni alijitesa vikali ili kuomba huruma ya Mwenyezi Mungu. Alijitesa kiasi kwamba alijipiga mijeledi mwishowe a...