Historia Rozari ni taji la Mawaridi.Ni neno la kilatini lenye maana ya Bustani ya maua ya waridi. Rozari inahusishwa na Zaburi 150 ambazo Wayahudi walizitumia kama sala hekaluni. Karne ya 12 walizuka wazushi wapinga dini, walioitwa Waalbigensia. Hawa walienea Kusini ya Ufaransa na Kaskazini ya Italia. Baba Mtakatifu wa wakati huo alimteua Padre Dominiki awahubirie. Aliwahubiria kwa maarifa yake yote lakini walizidi kushupaa na kumdhihaki. Mt.Dominiki alipoona kuwa uzito mkubwa wa dhambi walizotenda watu unazorotesha kuwageuza Waalbigensia, alikwenda msitu wa Toulouse na kusali mfululizo kwa siku tatu usiku na mchana. Akiwa msituni alijitesa vikali ili kuomba huruma ya Mwenyezi Mungu. Alijitesa kiasi kwamba alijipiga mijeledi mwishowe a...
Comments
Post a Comment